Pata habari Mbalimbali za Kitaifa na kimataifa, Breaking news,Elimu,Uchumi,Michezo,Siasa,Jamii, nk.. Jiunge nami kupitia Instagram,Facebook,Twitter,Youtube kwa jina moja la "Igp Mavala"

AJIRA ZA AFYA ZIMETOKA ANGALIA MAJINA NA VITUO WALIVYOPANGIWA


                     TANGAZO LA KUITWA KAZINI
 TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi
mbalimbali za kada za Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi
tarehe 30/08/2017 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi
umekamilika.
Aidha, mnatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi mlivyopangiwa katika muda
wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili mkiwa na vyeti halisi
(Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea
kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti
ya OR TAMISEMI www.tamisemi.go.tz. Hakutakuwa na mabadiliko ya vituo,
watakaoshindwa kuripoti katika muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na
waombaji wengine wa kada husika.
Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za
kazi zitakapotangazwa. Nafasi za Wauguzi na Wahudumu wa Afya
zitatangazwa mara baada ya kukamilisha zoezi la uchambuzi na uhakiki wa
vyeti.
Waajiri wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia
mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.
MkuuLimetolewa na:-
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
OR – TAMISEMI
30/10/2017
  FUNGUA HAPA KUONA MAJINA NA VITUO WALIVYOPANGIWA
http://tamisemi.go.tz/noticeboard/tangazo-1080-20171030-tangazo-la-kuitwa-kazini-na-orodha-waliopangiwa-vituo-vya-kazi/ORODHA_WALIOPANGWA_KWENYE_VITUO_VYA_KAZI.pdf
     @Igp Mavala
Powered by Blogger.