Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza kukutana Jumatatu tarehe 23 Oktoba
2017 Mjini Dodoma kutekeleza majukumu yake kabla ya kuanza kwa Mkutano
wa Tisa wa Bunge tarehe 7 Novemba 2017. Mhe. Spika Job Ndugai ameziita
Kamati hizo kuanza shughuli zake tarehe hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (3)
ya Kanuni za Kudumu za Bunge. Aidha, Mhe. Spika ameziita Kamati ya Masuala
ya UKIMWI, Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Kamati ya Hesabu
za Serikali (PAC) kuanza vikao vyake Oktoba 16, 2017.
Katika kipindi chote hiki, shughuli zilizopangwa kufanyika ni pamoja na kupokea,
kuchambua na kujadili taarifa kutoka Serikalini, taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uchambuzi wa Sheria Ndogo na uchambuzi
wa miswada mitatu ya sheria.
Kufuatia Tangazo hili, Wajumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI, Kamati ya
mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)
wanatakiwa kufika Dodoma tarehe 15 Oktoba, 2017 na Wajumbe wa Kamati
nyingine wafike Dodoma tarehe 22, Oktoba 2017. Ratiba ya vikao vya kwa kila
Kamati inapatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz.
@Igp Mavala