Pata habari Mbalimbali za Kitaifa na kimataifa, Breaking news,Elimu,Uchumi,Michezo,Siasa,Jamii, nk.. Jiunge nami kupitia Instagram,Facebook,Twitter,Youtube kwa jina moja la "Igp Mavala"

Antonio Conte kwenye kivuli cha Sir Alex Ferguson

Dimitri Berbatov aliwahi kukiri kwamba wakiwa mazoezini huwa kunatawala ukimya mkubwa kuanzia kwa wachezaji hadi makocha wengine wa benchi la ufundi pale kocha mkuu Sir Alex Ferguson anapofika Carrington.
Watu walikuwa wakimuogopa sana SAF japokuwa alikuwa anapenda kuwaweka wachezaji karibu na yeye, hakuna aliyekuwa juu ya Ferguson na ndio maana haikuwa jambo gumu mtu maarufu kama Beckham kuondoka United kwa style ya aibu.
Nimemkumbuka Alex Ferguson baada ya kumuona Antonio Conte anachowafanya Chelsea kwa sasa, bila uoga wala hofu yoyote anaingia katika msuguano na mchezaji mkubwa mwingine wa Chelsea tena ikiwa katika misimu miwili mfululizo.


Msimu uliopita Muitaliano huyu pamoja na msaada wote ambao Diego Costa aliutoa hadi Chelsea wakabeba ubingwa lakini Conte alimchana tena kwa message na kumuambia wazi hana mpango naye msimu huu.
Kila mtu alishtushwa na habari za Diego Costa lakini wakati watu wakiwa wameanza kusahau ya Diego Costa sasa Antonio Conte huyu huyu anaingia kwenye mzozo na mchezaji ambaye ni kipenzi cha mmiliki wa Chelsea Roman Abromovich.


Antonio Conte anajua wazi kwamba Roman ndio aling’ang’aniza David Luiz arudi Chelsea lakini Antonio anaziba macho na masikio anamuweka nje Luiz katika mechi kubwa na sababu ikitajwa kwamba ni kutokuelewana kati ya wawili hao.
Siku ya Alhamisi iliyopita Antonio Conte aliwaita wachezaji wote katika vyumba vya kubadilishia nguo na inadaiwa aliwapiha mkwara kuhusiana na masuala ya kufanya vitu asivyotaka na inadaiwa kwamba alimtumia Luiz kuonesha mfano kitakachowapata wengine.

Inasemekana katika mazoezi ya mwisho ya Chelsea kuelekea mchezo zidi ya Manchester United Conte alimuweka Luiz kama muokota mipira akishuhudia wenzie wakicheza mazoezi kati ya timu ya kwanza na ya akiba.
Wakati Antonio Conte huyu huyu anamtema Branislav Ivanovic kila mtu alijiuliza kuhusu akili za Conte lakini akambwaga bila kusikiliza ni ni watu au mashabiki wa Chelsea watasema.

Huyu ndio Conte mwenye roho ya Fergie hajali kuhusu bosi, hajali kuhusu umaarufu wako na jina lako anachotaka yeye kila mtu ajue kwamba yeye ndio kiongozi wa timu na usipomsikiliza utaokota mipira mazoezini kama David Luiz.

©®Igp Mavala
Powered by Blogger.