Pata habari Mbalimbali za Kitaifa na kimataifa, Breaking news,Elimu,Uchumi,Michezo,Siasa,Jamii, nk.. Jiunge nami kupitia Instagram,Facebook,Twitter,Youtube kwa jina moja la "Igp Mavala"

Huyu ndiye Himid Mao Mkami


Huyu ndiye Himid Mao Mkami "Ninja" mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza,Mtibwa ya Morogoro na Moro united ya Morogoro Mao Mkami "Ball dancer".

Himid alianza kucheza katika Academy ya Azam ya timu ya vijana iliyofanikiwa kutwaa ubingwa kombe la Uhai (Uhai Cup) mara mbili mfululizo.

Mwalimu wa zamani wa timu ya Taifa mbrazil Marcio Maximo alimuona kijana huyu akiwa  kwenye kituo cha kulea vipaji cha TFF  Tanzania Soccer Academy (TSA) alimuita National team ili kuleta changamoto kwenye kikosi chake hasa kwenye safu ya kiungo kwenye zama hizo za kina Henry Joseph,Shaban Nditi na Athuman Idd (Chuji).

Himid ndiye mchezaji pekee ambaye ameweza kuitumikia Azam fc kwa muda mrefu akiwepo John Bocco ambaye ametimkia Simba pamoja na Aboubakar Salum "Sureboy".Aliitenda kazi yake vilivyo akicheza kama kiungo mkabaji huku Domayo na Sureboy wakicheza mbele yake kama viungo washambuliaji.

Hatimaye Himid amekuwa kiungo tegemeo katika klabu yake na timu ya Taifa pia.Huyu ndiye kiungo mkabaji asilia (A holding midfield).Ni mzuri sana katika kucheza box to box.Kiungo huyu ambaye anaaminika kwa kucheza kindava na kutibua mipango ya timu pinzani na ni mzuri pia katika kuwalinda mabeki wake.Ni kiungo mwenye sifa zote za kucheza kwenye eneo la midfield.

Himid ana nguvu,umakini,discipline na ni mkomavu pia.Kwa muda ambao ameitumikia timu yake,tayari ametengeneza muunganiko mzuri na kiungo Salum Abubakar ambae amekua akicheza juu yake kama kiungo mshambuliaji.Wametengeneza pacha nzuri sana pale Azam Fc also kwenye timu ya Taifa Himid amekuwa mhimili mkubwa sana katika safu ya kiungo.Ameendelea kuaminiwa na Mwalimu Mayanga Salum akicheza kama holding na Mzamiru Yassin akicheza juu yake.Ni mchezaji ambaye amezidi kuthibitisha ubora wake kwenye klabu yake na timu ya Taifa.

Huyu ndiye kiungo mkabaji "mkata umeme" haswa.The way anavyo jituma uwanjani, umakini,nidhamu na ubora wake ni moja ya mambo yanayomfanya aaminiwe na walimu.Ni mchezaji wa mechi kubwa na mwenye utimamu wa mwili uwanjani pia amekuwa katika ubora wake kila game.

Bao lake dhidi ya Ruvu shooting lililoipa timu yake ubingwa wa league kwa mara ya kwanza, kadhalika lile shuti lake la mita 35 lililomtungua Daniel Agyei wa Simba kwenye fainal ya kombe la mapinduzi kule zanzibar na kuipa timu yake ubingwa wa Mapinduzi cup ni moja ya mafanikio ambayo hayata sahaulika kwa Himid dhidi ya timu yake.

Taifa bado linaitaji vijana wa kariba ya Himid kwa miaka ya usoni ili waweze kua msaada kwa soka letu.
©®Igp Mavala
+255769432919
Powered by Blogger.