Pata habari Mbalimbali za Kitaifa na kimataifa, Breaking news,Elimu,Uchumi,Michezo,Siasa,Jamii, nk.. Jiunge nami kupitia Instagram,Facebook,Twitter,Youtube kwa jina moja la "Igp Mavala"

Erasto Nyoni na Muzamiru kukosa Mechi Ya Taifa Stars

MABADILIKO TAIFA STARS:

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga amewaita kikosini viungo Jonas Mkude kutoka Simba na Mudathir Yahya wa Singida United.

Mkude na Mudathir wanachukuwa nafasi za Erasto Nyoni na Muzamiru Yassin wote kutoka Simba ambao awali walijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 walioitwa na Mayanga.

Kocha Mayanga amelazimika kuwaondoa kikosini Nyoni na Muzamiru baada ya taarifa ya ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusiana na kadi nyekundu walizopata wachezaji hao kwenye mchezo wa kirafiki uliopita.

Mchezo uliopita ulikuwa ni dhidi ya timu ya The Flames ya Malawi uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa FIFA, Nyoni na Muzamiru wataukosa mchezo ujao dhidi ya Benin kutokana na Kanuni za Nidhamu za FIFA ambako kifungu cha 18 (4) kinaelekeza mchezaji mwenye kadi nyekundu kuukosa mchezo unaofuata.

Kwa suala la mechi za kirafiki kifungu cha 38 (2) (g), kinatamka wazi kuwa mchezaji mwenye adhabu ya kadi nyekundu moja kwa moja anaukosa mchezo wa kirafiki unaofuata.

Kwa ufafanuzi huo wa FIFA, Mayanga amewaondoa Nyoni na Muzamiru kikosini ili kutumikia adhabu hiyo kwa mchezo unaofuata wa kirafiki na nafasi zao kujazwa na Mkude na Mudathir.

Wachezaji hao watajiunga kambini na wachezaji wengine walioitwa katika kambi ambayo imeshaanza Novemba 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Benin utakaochezwa kwenye tarehe za kwenye kalenda ya FIFA Novemba 12, huko Benin.

Wachezaji wengine wanaounda kikosi hicho kinachodhaminiwa na Bia ya Serengeti ni

Makipa –

1.      Aishi Manula

2.      Ramadhani Kabwili

3.      Peter Manyika

Walinzi Wa Pembeni

4.      Gadiel Michael

5.      Boniphas Maganga

Walinzi Wa Kati

6.      Abdi Banda

7.      Kelvin Yondani

8.      Nurdin Chona

9.      Dickson Job

Viungo Wa Kati

10.  Himid Mao

11.  Hamis Abdallah

12.  Raphael Daudi

13.  Mohamed Issa

Viungo Wa Pembeni

14.  Simon Msuva

15.  Shiza Kichuya

16.  Faridi Mussa

17.  Ibrahim Ajib

Washambuliaji

18.  Mbwana Samatta

19.  Mbaraka Yusuph

20.  Elias Maguli

21.  Yohana Mkomola

22.  Abdul Mohamed

©®Igp Mavala
Powered by Blogger.