TEWW YATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Ole Nasha ameitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kimuundo badala ya kufikiria kufanya miradi ambayo imekuwa ikiwaondoa kwenye mwelekeo wa malengo ya uanzishwaji wa Taasisi hiyo.
Naibu Waziri Ole Nasha ametoa wito huo jijini Dar es Salaam alipotembelea Taasisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuzitambua taasisi zilizo chini ya wizara pamoja na utendaji wa majukumu yake.
Akiwa katika Taasi hiyo amesema nchi bado inaihitaji Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima pamoja na aina ya elimu ambayo inatolewa na taasisi hiyo, hivyo ameitaka kuendelea kutekeleza majukumu yake ili iendane hali halisi ya mazingira ya elimu.
Ole Nasha amesema ukiangalia utekelezaji wa miradi hiyo inabaki kuitwa elimu ya watu wazima lakini namna inavyoendeshwa haziakisi uhalisia huo zinabaki kuwa kama mifumo mingine ya utoaji wa elimu ya mfumo rasmi
Naibu Waziri Ole Nasha akiwa katika Taasisi hiyo amepata fursa ya kutembelea chumba cha Uchapaji vitabu na majarida, Karakana, Maktaba na Idara ya Elimu Masafa na Studio za kuandaa vipindi vya kuelimisha umma vya Elimu ya Watu Wazima.
Aidha, Naibu Waziri ametembelea Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Elimu, Habari na Utamaduni ya UNESCO na kuwataka kuitisha kikao cha wadau wanaohusika na Tume hiyo ili kuzungumzia changamoto za kimfumo na muundo zinazoikabili taasisi hiyo.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
31/10/2017
@Igp Mavala
@Igp Mavala