Pata habari Mbalimbali za Kitaifa na kimataifa, Breaking news,Elimu,Uchumi,Michezo,Siasa,Jamii, nk.. Jiunge nami kupitia Instagram,Facebook,Twitter,Youtube kwa jina moja la "Igp Mavala"

Mbunge Hussein Bashe "MIMI SIYO WA NDIYO MZEE"





Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amefunguka na kusema wakati anaomba kura na Mhe. Rais Dkt. Magufuli mwaka 2015 alimwambia kiongozi huyo kuwa yeye hawezi kwenda bungeni na kuwa kati ya wale wabunge wa kusema 'Ndiyo' mzee.

Bashe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na wananchi wa jimbo la Nzega akiwaeleza mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika miaka miwili jimboni hapo toka alipochaguliwa kuwa Mbunge Oktoba 25, 2015.   
"Mimi nikienda Bungeni nikisimama naposema nasema kweli kwa sababu kiapo cha CCM kinasema 'daima nitasema kweli unafiki kwangu mwiko' huo ndio msimamo wangu na siku naona kura na Mhe. Rais nilimwambia Rais jukwaani kwamba Mhe. Rais mimi siendi kuwa Mbunge wa ndio mzee bali mimi naenda kutimiza wajibu wangu na wajibu wangu ni kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali"alisema Bashe 
Aidha Mbunge huyo alisema ataendelea kubaki na msimamo wake huo wa kuisimamia serikali labda mpaka wazee wa jimboni kwake wamshauri vinginevyo ili na yeye akiingia akae kimya avute pesa na kutulia kimya. 
"Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM huwezi kumuachia mtoto wa jirani kutatua matatizo ya ndani ya nyumba yenu na huo ndiyo msimamo wangu lakini wazee mkisema baba eeh wewe nenda kawa mzee wa ndiyo mzee, zikija vuta saini nenda zako mtaani basi nitafanya hivyo kwa sababu nitakula good time kama wabunge wengine" alisisitiza Bashe 
Mbali na hilo Bashe amewaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa wanapoelekea mwaka wa 2020 kuwa changamoto ya maji, umeme itakuwa historia jimboni hapo na kusema katika suala la elimu watahakikisha wanafika kiwango ambacho watajivunia.  

@Igp Mavala
Powered by Blogger.