Maskini Neymar, aangua kilio mbele ya waandishi wa habari
Baada ya Brazil kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 3 dhidi ya Japan kulikuwa na mkutano baada ya mechi kati ya waandishi wa habari na nahodha wa Brazil Neymar pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo Tite.
Katika mkutano huo jambo lililovuta hisia na kusikitisha mashabiki wa Brazil na PSG ni kitendo cha Mbrazil Neymar Dos Santos kuangua kilio na kisha kuamua kuondoka katika chumba cha mkutano.
Neymar aliangua kilio wakati kocha wake Tite akimzungumzia na akimtetea kuhusu habari zinazoandikwa siku za usoni kwamba hana furaha na maisha ya PSG na uhusiano wake na kocha wa klabu hiyo sio mzuri.
Tite amesema anakerwa sana na habari anazozishiwa Neymar ikiwemo kuwa na mahusiano mabaya na yeye kwani hajawahi kugombana na Neymar, wakati Tite akiendelea kumtetea Neymar ndipo alianza kulia.
eymar mwenyewe kabla ya Tite kuongea alisisitiza kwamba ana furaha kuwa katika klabu ya PSG na kusema kwamba hana tatizo na mchezaji yoyote katika klabu hiyo, na yuko vizuri tu na Edison Cavani.
Alisisitiza kwamba kitu pekee kinamsumbua kwa sasa na kuambiwa hayuko vizuri na Edison Cavanni na amewataka waandishi wa habari kuacha kutunga story na kuandika vitu wasivyovijua.
Neymar alisajiliwa na PSG akitokea Barcelona kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya £198m lakini tangu atue PSG amekuwa akitengeneza vichwa vingi vya habari na vingi vikiwa sio vizuri.
©®Igp Mavala