MASKINI MOHAMMED IBRAHIM 'MO' NA KIPAJI CHAKE.
Alikuwa ni sehemu ya mafanikio ya mfumo aliokuwa anatumia Mcameroon Joseph Marius Omog kutokana na mbinu yake ya kushambulia kupita katikati.Na hiyo ilikuwa ni kabla ya ujio wa Mganda Emmanuel Okwi pale msimbazi.
Mohamed Ibrahim 'Mo' alikuwa anafit pale mbele na Joseph Omog alikuwa akimchezesha either kama kiungo mshambuliaji au wing ya pembeni upande wa kushoto.Alikuwa anacheza pacha nzuri sana na Mzamiru Yassin.
Ni mchezaji mjanja na mwenye timming haswa,anajua kuwasoma mabeki na ni mwepesi kuelewa positioning ya mlinda lango.Ana nguvu miguuni na ana jicho la mpira.Ni mzuri katika dribbling,shouting na assisting.'Mo' aki dribble kama mbili na aka aticipate kidogo, hakika hakuachi.
Akicheza kama kiungo mshambuliaji kutoka pembeni hasa kule kushoto na kulia ukamkuta Ramadhani Kichuya,hapo Mzamiru anakuwa kama link hakika ilikuwa ni combination nzuri iliyojengeka kwa muda mrefu kidogo.
Ujio wa mastraika John Raphael Bocco, Emanuel Okwi na Mghana Nicolas Gyan umempoteza huyu kijana.Alianza kutokea sub na sometimes amekuwa hagusi kabisa.
Ni kipindi ambacho ubora wa viungo ulithibitika pale Simba,Mkude Jonas,James Kotei,Mzamiru Yassin,Mohammed Ibrahim,Shizza Kichuya, Jamali Mnyate na Said Ndemla.Ilikuwa ni kipindi ambacho simba iliperfom kwenye league bila kutegemea mshambuliaji wa mwisho (a top straicker).
Ni kipaji ambacho kinaenda kupotea hivi hivi, kama alivyo Juma Mahadhi pale Yanga akitokea Cost ya Tanga.Kijana ambae wengi tuliamini kuwa anauwezo wa ku compete na Msuva Simon.Hatimaye kapotea kabisa,Msuva katimkia zake ughaibuni lakini Mahadhi hata mara pengine sub hayumo.Hizo dalili zimeanza kuonekana kwa 'Mo' benchi imekuwa maisha ya huyu mdogo wangu.
Niliamini kwamba huyu na Mzamiru Yassin wangekuwa tegemeo sana kwa soka letu kama ilivyo kwa Samatta,Msuva na Banda.
Bado nalilia kipaji cha huyu kijana, hakika hakuna mtanzania mpenda soka anaye furahia kupotea kwa kijana cha huyu kijana aliye thibitisha ubora wake kwa muda ambao amecheza pale Simba.
~…Mwisho
©®Igp Mavala