Pata habari Mbalimbali za Kitaifa na kimataifa, Breaking news,Elimu,Uchumi,Michezo,Siasa,Jamii, nk.. Jiunge nami kupitia Instagram,Facebook,Twitter,Youtube kwa jina moja la "Igp Mavala"

MWANAFUNZI MWENYE MIMBA AKAMATWE YEYE NA WAZAZI WAKE HADI AMTAJE MHUSIKA:

Exclusively:

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa shule kwenye mkoa huo, kumkamata na kuwaweka ndani Mzazi na Mwanafunzi yeyote wa kike atakayebainika kuwa na mimba hadi hapo watakapomtaja anaehusika na mimba hiyo.

Amesema kumekuwa na tabia ya kumalizana kienyeji huko majumbani na matokeo yake Watuhumiwa hawafikishwi sehemu husika ili waweze kuwajibishwa.

“Mwalimu Mkuu unapogundua Mwananfunzi ana mimba mweke pembeni ita Wazazi wake, washirikishe polisi wawachukue wawekwe ndani kwa muda wa saa 48 hadi hapo watakapomtaja Muhusika wa mimba hiyo, ukifanya hivyo mara kadhaa mabadiliko yatatokea,” Amesisitiza

Ametoa agizo hilo baada ya kusomewa taarifa ya Shule ya sekondari Kirando kwenye Wilaya ya Nkasi wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa maabara pamoja na kuongea na Wanafunzi, na kupewa taarifa ya mimba saba kwa kipindi cha January hadi October mwaka huu wa 2017 na kesi zote zipo polisi.

Alitahadharisha kuwa shule yeyote atakayoitembelea katika ziara yake hiyo ya kujitambulisha katika Halmashauri nne za mkoa huo, ihakikishe inabainisha hatua zilizochukuliwa kwa Watuhumiwa na zilipofikia na si kueleza tu idadi ya kesi na kuwepo kwa kesi hizo polisi.

Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kirando Erneo Mgina amesema kuwa kati ya Wanafunzi saba waliopata ujauzito Wanafunzi watatu ni wa “A – Level” na wanne ni wa “O – Level” na kueleza kuwa wengi wao hupata mimba wakati wa likizo na huwabaini pale tu wanaporudi shule na kuwapima.

©®Igp Mavala
Powered by Blogger.