Pata habari Mbalimbali za Kitaifa na kimataifa, Breaking news,Elimu,Uchumi,Michezo,Siasa,Jamii, nk.. Jiunge nami kupitia Instagram,Facebook,Twitter,Youtube kwa jina moja la "Igp Mavala"

Mahakama yamwachia huru Kigogo wa ESCROW.

Ni habari kutoka Mahakamani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam leo November 2 2017 ambapo mmoja wa ‘vigogo’ kwenye sakata la ESCROW ameachiwa huru.
millardayo.com na AyoTV zinaripoti kwamba Mahakama hiyo ya Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma ambae alikua anakabiliwa na kosa la kupokea rushwa ya Sh. milioni 323 kutoka kwa MfanyabiasharaJames Rugemalira.
Taarifa inaeleza zaidi kwamba fedha hizo zilikua ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW ambapo kigogo huyo ameachiwa na hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa TAKUKURU, Leonard Swai kuomba kesi hiyo iondolewe Mahakamani chini ya kifungu cha 98 (a) cha  sheria ya Makosa ya Jinai (CPA).
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alisema Mshtakiwa huyo amefutiwa kesi na kwa sasa yupo huru ambapo kama utakumbuka, Rugonzibwa alifikishwa Mahakamani kwa Mara ya kwanza January 14, 2015 na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU).
Inadaiwa alipokea rushwa hiyo ya milioni 323 kutoka kwa Rugemalira ambae alikuwa ni mshauri huru wa kitaalamu, Mkurugenzi wa VIP na mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa kampuni hiyo.

Cc Mallard Ayo. Com
@Igp Mavala
Powered by Blogger.