Manchester City ndo club yenye kikosi ghali zaid duniani
Utafiti uliofanya na shirika la CIES Football Obsevatory unaonesha vilabu vya nchini Uingereza Manchester City na Tottenham ndio vilabu vinavyoongoza kuwa na kikosi chenye thamani kubwa ulimwenguni.
Ripoti ya utafiti huo inasema Man City kikosi chao cha kwanza kuna wachezaji wanne ambao kwa sasa kama wataamua kuwauza baasi thamani yao lazima itakuwa ni kuanzia kiasi cha €100m.
Mchezaji wa Manchester City ambaye kwa sasa ukimuweka sokoni ana thamani kubwa zaidi ni Kelvin De Bruyne ambaye mauzo yake sokoni yanaweza kuwa €145m akifuatiwa na Leroy Sane €119.5m.
Raheem Sterling thamani yake imepanda hadi kufikia €118.2m huku kuna Gabriel Jesus ambaye thamani yake sokoni ni €107m ambalo kwa ujumla pamoja na wachezaji wengine Manchester City wana thamani ya €1.19b.
Tottenham Hotspur kikosi chao thamani yake ni €1.17bn huku Harry Kane pekee thamani yake ni €185.6m, Delle Ali €181.7m na hii inamaanisha kwenye 3 bora ya wachezaji wenye thamani duniani Tottenham ina wachezaji wawili.
Ukimuacha Ali na Kane yupo Eriksen €104.9m yupo Heung Son Min €67.5m. Barcelona wanafuatia katika nafasi ya 3 wana Lioneil Messi €117.3m wana Luis Suarez 133.6m na kwa ujumla kikosi chao kina thamani ya €1.13bn.
Chelsea wapo katika nafasi ya nne ambapo kikosi chao kina thamani ya €1.04bn huku Manchester United wakiwa ya 5 na £812.9bn lakini Romelu Lukaku(€165m) ametajwa kuwa na thamani kubwa kuliko Messi, Ronaldo na Hazard.
Real Madrid wako nafasi ya 6 huku bei ya Cr7 ikishuka hadi kufikia €96m akipitwa hadi na Mohamed Salah ambaye yeye na Liverpool wako nafasi ya 7 lakini Mo Salah mwenyewe ana thamani ya €101m.
Cc Shafih dauda
©®Igp mavala
Ripoti hii ya CIES mara nyingi huwa inaangalia viwango vya wachezaji wanapokuwa uwanjani lakini vile vile umri huwa ni kigezo kikubwa na kile wanachofanya uwanjani katika kipindi ambacho ripoti inaandikwa.